Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma • May 29, 2026

MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM WA TAIFA

Uniting Leaders, Delegates, and Citizens for Progress

About CCM

Discover our story and explore the key drivers shaping this initiative

About

Mkutano Mkuu Maalum wa Kitaifa wa CCM ni tukio muhimu lililoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuwakutanisha wanachama wa chama, viongozi, pamoja na wageni waalikwa kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Mkutano huu unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, Dodoma, tarehe 29–30 Mei 2025.

Lengo kuu la Mkutano huu ni kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020, kupendekeza marekebisho madogo ya Katiba ya CCM (Toleo la Januari 2025), pamoja na kuzindua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025–2030.

Mkutano huu unatoa jukwaa kwa wajumbe kushiriki katika mijadala ya kikatiba, kisiasa na kimkakati, huku ukihakikisha kuwa maandalizi yote ya kiutendaji, afya na usalama yanawekwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha ushiriki wenye tija na ufanisi.

Kupitia Mkutano huu, CCM inathibitisha upya dhamira yake ya kuendeleza maendeleo ya Taifa, kuimarisha umoja wa kitaifa, na kuendeleza utawala bora kwa kushirikisha viongozi, wajumbe na wananchi kwa ujumla.

Services & Logistics

Taarifa muhimu kwa ajili ya kushiriki tukio kwa urahisi na ufanisi

  • (i) Wajumbe kutoka mikoa mingine watapokelewa Makao Makuu ya CCM Dodoma na kupelekwa maeneo ya malazi.
  • (ii) Mapokezi yataratibiwa na Kamati ya Itifaki na Mapokezi kwa kushirikiana na wajitolea.
  • (iii) Vitambulisho vitatolewa na Sekretarieti mara baada ya kuwasili.
  • (iv) Makatibu wa Mikoa watagawa vitambulisho kwa wajumbe wao kabla ya kuanza kwa mkutano.

Malipo ya posho yatafanyika moja kwa moja kwenye akaunti za benki za wajumbe kama zilivyowasilishwa na mikoa yao. Posho za wageni zitasimamiwa na Timu za Fedha na Itifaki.

Chakula na vinywaji vitatolewa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, vikihudumiwa na kampuni zilizoidhinishwa.

Huduma ya kwanza ya afya (First Aid) itapatikana katika eneo la tukio. Wajumbe wanashauriwa kuchukua tahadhari za kiafya wakati wa tukio na baada ya kumalizika.

Usalama ni jukumu la kila mshiriki. Eneo la mkutano na malazi yanalindwa ipasavyo. Epuka kutembea peke yako nyakati za usiku.

Malazi yameandaliwa kwa wajumbe na baadhi ya wageni kwa kipindi cha siku 3 (tarehe 28–30 Mei 2025). Taarifa kamili za hoteli, vyumba na maeneo zitatolewa kulingana na mikoa.

Wajumbe wanatakiwa kuvaa mavazi rasmi ya Chama: shati la kijani na suruali au sketi nyeusi. Kumbuka hali ya baridi wakati wa usiku Dodoma; vaa mavazi yanayofaa.

Huduma za kifedha zinapatikana nje ya eneo la tukio. Huduma za mitandao ya simu na benki zinazopatikana ni pamoja na M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, PBZ, NMB na CRDB.

Maeneo maalum ya ibada na sala kwa madhehebu yote yameandaliwa nje ya ukumbi mkuu wa mkutano.

Meeting Program

07:30 – 08:45
Wajumbe na waalikwa kuingia Ukumbini.
  • Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo/ Makatibu wa Mikoa
Viongozi kuwasili Ukumbini.
  • Naibu Katibu Mkuu Bara/ Zanzibar
08:45 – 09:00
09:00 – 09:05
Mwenyekiti wa CCM kuwasili Ukumbini
  • Katibu Mkuu wa CCM
Wimbo wa Taifa. Wimbo wa Afrika Mashariki.
  • Katibu Mkuu wa CCM.
09:15 – 09:25

Contact Us

Reach out to us for any inquiries.